Followers

Shule Yatangaza Kuruhusu Wanafunzi wa Kiume Kuvaa Sketi

Shule moja ya bweni nchini Uingereza ijulikanayo kama Uppingham School imetangaza kuruhusu wanafunzi wa kiume wa shule hiyo kuvaa sketi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Richard Maloney ameeleza kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakayeomba ruhusa ya kuvaa sketi ataruhusiwa kwani anaamini uhuru na uchaguzi wa mtu ni lazima viheshimiwe.

Inaelezwa kuwa suala hili la kuvaa uniform ya aina yoyote kutasaidia sana katika kuondoa ubaguzi wa kijinsia baina ya wanafunzi.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.