Followers

Spika Wa Bunge Ndugai Arejea Kwa Kishindo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, leo Aprili 9, 2018 amerejea Bungeni na kuendesha kikao cha tano cha Bunge, baada ya muda mrefu wa kuwa nje ya nchi kwa matibabu.

Tukio la Ndugai kurejea Bungeni lilifurahiwa na wabunge wengi huku wakielezea hisia zao, na kumshukuru Mungu kwa kuweza kuungana nao tena.

Spika Ndugai alikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili akiwa kwenye matibabu, huku kukiwa na tetesi kuwa alikuwa akiumwa sana, lakini amerejea hivi karibuni akiwa na afya njema na kuendelea na majukumu yake ya Bunge

Download app ya supernida kupata habari zote kiganjani Mwako

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.