Followers

Ufahamu Ugonjwa wa Kichocho kwa Undani


Kichocho ni ugonjwa ambao huathiri eneo fulani la jamii au eneo fulani la kijiografia kwa kitaalamu tunaita endemic, ambapo watu wanaathirika kutokana na shughuli zao za kila siku mfano wakulima, wavuvi, na vilevile kutokana na starehe kama kuogelea kweye bwawa lisilo salama au ziwani.
Kichocho huambukizwaje?
Maambukizi ya ugonjwa huu wa kichocho hutokea pale mabuu (larvae) ya vimelea vya shistosoma yalioachiwa kutoka kwa konokono wa majini yanapopenya ngozi ya mtu aliye kwenye maji yalioathiriwa.

Ndani ya mwili wa binadamu haya mabuu (larvae) huendelea kukomaa na kuwa vimelea kamili, vimelea hivi hupenda kuishi kwenye mishipa ya damu, vimelea jike hutaga mayai, ambapo baadhi ya mayai hutolewa kwa kukojoa au kwa njia ya haja kubwa. Na mzunguko huendelea.
Aina za kichocho
Kuna aina mbili za kichocho ambazo ni:

1. Kichocho cha utumbo ama intestinal schistosomiasis.
2. Kichocho cha mfumo wa mkojo ama urinary schistosomiaisis.

Kila aina ya kichocho kinaletwa na aina tofauti za vimelea hawa wa schistosoma kama ifuatavyo:
• Kichocho cha Utumbo (Intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea vya Schistosoma mansoni na Schistosoma intercalatum
Kichocho cha Utumbo aina ya Asia (asian intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea aina ya Schistosoma japonicum na Schistosoma mekongi.

•Kichocho cha mkojo (Urinary schistosomiasis) husababishwa na vimelea jamii ya Schistosoma hematobium.

Dalili za kichocho

Maumivu ya tumbo.Kuhara damu hasa kwa kichocho cha utumbo.Kukojoa damu (terminal hematuria) hasa kwa kichocho cha mkojo.KikohoziHomaUchovuNgozi kuwasha (cercarial dermatitis) kwa jina lingine swimmers itch.

Vipimo na Uchunguzi

Kuangalia uwepo wa mayai ya vimelea kwenye mkojo na kinyesi kwa kutumia Hadubini.X-ray ya tumbo.Ultrasound ya tumbo.Kipimo cha damu (complete blood count).Cystoscopy kwa kichocho cha mkojo

Sigmoidoscopy/proctoscopy kwa kichocho cha utumbo.

Matibabu
Kichocho hutibiwa kwa kutumia dozi ya mara moja ya dawa iitwayo Praziquantel.

Madhara ya Kichocho 
Kansa ya kibofu cha mkojo (cancer of urinary bladder).Figo kushindwa kufanya kazi Cor pulmonale.Gastrointestinal bleeding - Kuvuja damu ndani ya mwili hasa katika mfumo mzima wa chakula.Portal hypertension.Seizures - Kifafa au degedege.Reflex nephropathy.

Jinsi ya kuzuia kichocho

Kuondoa na kuangamiza konokono waliopo kwenye maji au ambao hupenda kuishi kwenye maji ambao ni muhimu katika mzunguko wa kuuwaji wa vimelea vinavyoleta kichocho kwa kutumia Acrolein, copper sulfate na niclosamide.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.