Wakili wa ACT Wazalendo amekamatwa na Polisi kwa kuwatetea Madiwani
Jana April 1, 2018 Mjumbe wa Kamati Kuu, na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Sheria ya ACT Wazalendo, Wakili Thomas Msasa amekamatwa na polisi jana mjini Kigoma kwa sababu ya kuwatetea Madiwani, Viongozi na Wanachama wa Chama hicho waliokuwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Kigoma, Sendwe Ibrahimu Mbaruku imesema Wakili Msasa alikwenda polisi kama Wakili wa Madiwani wawili wa ACT Wazalendo, Diwani wa Kata ya Kipampa, Mussa Mgongolwa, pamoja na Diwani wa Kata ya Kigoma, Hussein Kalyango, aliyekuwa mgombea Udiwani Kata ya Mwanga Winston Mogha, Katibu wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Mkoa, Masabo, pamoja na wanachama na wafuasi mbalimbali wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Kigoma.
“Kukamatwa huku ni sehemu ya mpango wa CCM na Jeshi la Polisi wa kukamata Viongozi na Wafuasi wa Vyama vya Upinzani unaoendelea nchi nzima, na kuhakikisha kuwa wanawaweka ndani kwa muda mrefu kwa uonevu tu.” –Mwenyekiti Mbaruku
“Chama ngazi ya Mkoa, pamoja na Taifa tunashirikiana kuhakikisha wote waliokamatwa wanaachiwa au wanafikishwa mahakamani.” -Mwenyekiti Mbaruku
No comments
Post a Comment