WATU4 WAFARIKI DUNIA MKOANI TABORA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mfululizo ukanda huu wa Afrika mashariki, Watu wanne wamepoteza maisha kwa maeneo tofauti Wilayani Nzega mkoani Tabora
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbrod Mutafungwa amesema kua watu watatu waliangukiwa na nyumba aina ya Tembe( Nyumba yenye kufunikwa na Udongo juu) waliyokua wamelala usiku wa Tarehe 16/04/2018 majira ya saa9 usiku akiwataja kwa majina marehemu hao wa familia moja Tatu Selemani umri[28] akiwa na watoto Nassi Majuto umri [4] na Seleman Kafuku umri[4] katika kijiji cha Milambo kata ya Puge tarafa ya Itobo wilayani Nzega mkoa wa Tabora
Tukio lingine limetokea usiku wa leo tarehe 17 April 2018 katika kijiji cha Sigiri katikati ya Wilaya ya Nzega na Kahama Mathiasi Malali mwenye umri [48] Mwinjiristi wa kanisa la KKKT akiwa amelala na mkewe waliangukiwa na ukuta na kupelekea kifo cha mtu huyo na Mkewe kujeruhiwa mwili wake alikimbizwa hospitali ya wilaya ya Nzega na anaendelea na matibabu hali yake inaendelea kua vizuri
Kamanda Mutafungwa waasa wananchi wote kuhakikisha wanachukua tahadhari mapema pindi wanapoona mazingira ya makazi yamekua hatarishi na kwa wale wanaoishi sehemu za mabondeni na sehemu za njia ya maji kuchukua hatua mapema kabla madhara hayajatokea.
No comments
Post a Comment