Followers

Bungeni:Wabunge wahofia kupanda bei za Mafuta mwezi wa Ramadhani



Imewekwa Tarehe May 7, 2018

Wabunge wa CCM, Juma Nkamia (Chemba) na Hussein Bashe (Nzega Mjini), wameitaka Serikali kushughulia kupanda bei za Mafuta kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma, Nkamia aliomba Mwongozo kuhusu  mafuta na Bashe kutaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge kwa dakika 30 ili kujadili suala la kodi ya tende ili iondolewe kama ilivyo kwa nchi jirani.

Nkamia alisema katika baadhi ya vyombo vya habari kuna taarifa za kuadimika kwa mafuta ya kula hali hii inasababisha  mafuta kupanda bei kwa haraka.

Akijibu Mwongozo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema tatizo lililojitokeza ni suala la kodi kwani kwa sasa Taifa lina hifadhi ya mafuta ghafi tani 40,000 na meli zilizopo nje zina tani 50,000.

Amesema Jumla zilizoko nje na ndani  zina tani 90,000. Kinachoweka tatizo ni kodi kwa sheria tulizopitisha Tanzania, tunatoza kodi (meli kutoka nje ya nchi) asilimia 10 kwa mafuta ghafi.

Ameongeza kuwa vipimo vinaonyesha si mafuta ghafi ni mafuta masafi hivyo wanataka kutoza asilimia 25 na hapo ndipo kuna tatizo la hadi kufikia leo au kesho watatoa majibu ya walipofikia.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.