Followers

Mzambia kaacha jina la Mrundi



Hata hivyo, Lwandamina hakufahamu kuwa anaweza kuondoka fasta ndani ya Yanga wakati mkataba wake ukiwa haujamalizika na timu ikiendelea na michuano ya kimataifa.

MZAMBIA George Lwandamina ameanza kutoa huduma yake kwenye kikosi Zesco United, lakini inafahamika kuwa aliacha ripoti ya kuhitaji straika mmoja matata kwa ajili ya msimu ujao.

Hata hivyo, Lwandamina hakufahamu kuwa anaweza kuondoka fasta ndani ya Yanga wakati mkataba wake ukiwa haujamalizika na timu ikiendelea na michuano ya kimataifa.

Lakini, Mwanaspoti linafahamu kuwa jina la straika wa Stand United, Blaise Bigirimana ndio liliachwa kwenye ripoti ya Lwandamina akitaka kuongezwa kwenye safu ya ushambuliaji.

“Nikiwa pale nilikuwa nataka mastraika wawili wa nje na ndani mmoja, kuna yule mrefu wa Stand United (Birigimana) na Adam Salamba na Marcel, lakini nilitaka kuwaangalia hadi mwishoni mwa msimu.

“Yule Mrundi licha ya kuwa mrefu, lakini anajua kutembea na mpira vizuri, ana spidi na uwezo wa kupiga mashuti ni aina ya mshambuliaji aliyekosekana pale Yanga kwa sasa. Anajua kupambana uwanjani,” alisema. Kuhusu ripoti yake nusu aliyoiacha, alisema hilo ni jukumu la aliyekuwa kocha wake msaidizi (Mwandila), kumshauri kocha mpya Mwinyi Zahera kama ataweza kuitumia kuimarisha kikosi chao.

“Yule ni muajiriwa na yupo chini ya kocha mwingine, lakini ripoti nakumbuka nilimtumia kama akiifata itakuwa vizuri kwa Yanga msimu ujao na sio hao kuna sehemu zingine pia anajua nini cha kurekebishwa,” alisema. Mwanaspoti halikuishia hapo likaendelea kudodosa ndani ya Yanga na kuzungumza na mmoja wa Wajumbe katika kamati ya Utendaji, aliliambia Mwanaspoti, kweli majina hayo yalifika kwao ila bado wanaangalia namna ya kumalizana nao.

“Unajua pale iliposikika Yanga wanamtaka Salamba walijua labda ni baada ya kuifunga Simba, sio kweli jina lake lilikuwepo kabla Lwandamina hajaondoka, Marcel na Birigimana nayo yapo,” alisema kigogo huyo.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.