Followers

Kesi ya Mbowe, vigogo Chadema yaanza kusikilizwa


Dar es Salaam. Kesi ya kula njama na kufanya mikusanyiko isiyokuwa ya halali inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe imeanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakati kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikianza kusikilizwa, mshtakiwa wa saba, Halima Mdee na mshtakiwa wa tisa Ester Bulaya hawapo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala ameieleza Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri,  kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo mahakamani imetokana na usafiri waliokuwa wanatumia kutoka bungeni mjini Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuwa na tatizo na kusababisha wachelewe kufika.

Mbali na Mbowe ,washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa; naibu makatibu wakuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara) ambaye pia ni mbunge wa Kibamba.

Wengine, mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12  katika kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kufanya mkusanyiko usio halali ama

maandamano yaliyosababisha  kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.