Man United waishindwa rekodi ya Arsenal
Klabu ya soka ya Chelsea baada ya kuvuliwa ubingwa wake wa ligi kuu soka nchini England na Manchester City, hatimaye imejifariji kwa ubingwa wa Kombe kongwe nchini humo la FA.
Chelsea imewafunga Manchester United kwa bao 1-0 kwenye fainali iliyomalizika usiku huu kwenye uwanja wa Wembley jijini London na kufanya kombe hilo kubaki jijini humo likihama kutoka Emirates hadi Stamford Bridge.
Bao la Chelsea lilipatikana kupitia mkwaju wa penati dakika ya 22, likifungwa na nyota wa Ubeligji Eden Hazard ambaye aliangushwa na mlinzi Phil Jones wa Man United kwenye eneo la hatari.
Kwa ushindi huu Chelsea wameepuka kufuata rekodi ya Newcastle United mwaka 1998 na 1999 ilipofungwa fainali mara mbili mfululizo. Chelsea nayo msimu uliopita ilipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Arsenal.
Mancheter United wao wameshindwa kufikia rekodi ya Arsenal ya kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ambayo ni mara 13. Baada ya kufungwa wamebaki na ubingwa wao mara 12 huku wakicheza fainali mara 20 sawa na Arsenal.
No comments
Post a Comment