Followers

BREAKING NEWS: JESHI LA POLISI MKOANI TABORA LAWAKAMATA MAJAMBAZI 5 WALIOHUSIKA NA TUKIO LA KUMVAMIA MFANYABIASHARA NA KUPORA ZAIDI YA MILLION 39

Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa

Ikumbukwe kwamba tukio la kuvamiwa mfanyabiashara huyu aitwaye OMARY RAMADHAN KWAYI lilitokea tarehe 31/05/2018  maeneo ya mtaa wa Mwayunge  Wilaya ya Igunga Mkoa wa TABORA ambapo majambazi yalimvamia nyumbani kwake na kumpora pesa taslimu Tshs 39,800,000/= pamoja na simu aina ya TECNO yenye thamani ya Tsh 370,000/=

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Tabora lilifanya uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata majambazi watano ambao walikutwa wakiwa na mali mbalimbali ambazo ziliibwa katika tukio hilo

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Tabora SACP WILBROD MUTAFUNGWA amewataja majambazi hao kwa majina ya  MSABAHA RAMADHANI HASSAN, Miaka 32,Mkazi wa Igunga huyu ni ndugu wa Mfanyabiashara huyo, IBRAHIMU MUHAMED, Miaka 38 huyu ni Mfanyabiashara mwenzie, KISUDA RAMADHAN HASSAN, Miaka 40, Mkazi wa Manyoni – huyu ni Kaka yake na Mfanyabiashara huyo, MBOYI KISUDA, Miaka 28, Mkazi wa Manyoni na  GODFREY NJAU,Miaka 33, Mkazi wa manyoni.

Majambazi hao wamekamatwa na Pesa kiasi cha Tshs 4,600,000/= pamoja na simu aina ya TECNO ambayo ni mali ya mfanyabiashara huyo ambayo nayo iliibiwa katika tukio hilo.

Akifafanua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamanda MUTAFUNGWA amesema watuhumiwa wote watano wamehojiwa na wamekiri kuhusika na tukio hilo na juhudi zinaendelea ili kuweza kuzipata pesa nyingine zilizoibwa.

Vilevile Kamanda MUTAFUNGWA ameendelea kutuma salamu kwa Wahalifu na wenye nia yakuja kufanya uhalifu mkoa wa Tabora watafute shughuli nyingine yakufanya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora halifumbi Macho hata dakika moja muda wote liko kazini masaa24 

Kwa upande mwingine Kamanda MUTAFUNGWA amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ili kufichua wahalifu na uhalifu.

Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.