Je kunavita yatatu ya Dunia?? Hakuna vita kuu ya tatu:
Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa
WASIWASI kuwa kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Israel kwenda Yerusalemu ni mwanzo wa machafuko makubwa ambayo yangeisukuma dunia kwenda katika vita vingine vikubwa umeanza kukauka,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres. PICHA: MTANDAO
....kwani hali hiyo iliishia katika maandamano, tena ya vijana wadogo, kutaka kuvunja mpaka kati ya Gaza na Israel.
Hata umati wa watu Gaza haukujiunga na maandamano hayo, na eneo la Mashariki (Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan) ulibaki tulivu, na uongozi wa Palestina chini ya Rais Mahmud Abbas, licha ya kupinga kwa nguvu zote kuhamishwa ubalozi huo, na kuchukizwa na mauaji ya vijana wanaoandamana Gaza, hakuwaambia watu wake wajiunge na maandamano hayo. Ni kuikubali hali halisi.
Ukitazama tu vichwa vya habari utadhani kuwa ni tukio kama jingine lakini kuna dalili kuwa haya siyo matukio ya kawaida bali ni uyakinishaji na urasimishaji wa dola ya Israel kama ilivyo tangu kumalizika kwa vita vya siku sita vya Mashariki ya Kati, mwanzo wa mwezi Juni, 1967.
Ni miaka 51 tangu vita hivyo vipiganwe ambako sura ya Israel ilivyo sasa ilifikiwa, kwa njia ya kipingamizi cha kimantiki, kuwa nchi za Kiarabu zilijitupa kuiteketeza Israel finyu iliyoundwa mwaka 1947-8, ikiwa na ‘kidole’ kuingia Yerusalemu, huku eneo lililobaki likiwa ni la Wapalestina.
Endapo wangekubali maazimio ya Umoja wa Mataifa wakati huo, Wapalestina wangeunda nchi huru na mji wake mkuu ukiwa ni upande wa Mashariki wa Yerusalemu, kwani ule wa Magharibi ulitekwa na vikosi vya Wayahudi wakati Israel inaundwa kivita.
Ina maana Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 242, ambalo linaitaka Israel kurudi katika mipaka yake ya kabla ya kuanza vita ya Juni 1967, ni kama kuitaka Israel kupuuzia kuwa nchi za Kiarabu, zikiwa zinajua mipaka ilivyo na kuipuuza kutaka Israel ifutiliwe mbali, sasa zisamehewe kwa makosa hayo na Israel irudi katika mipaka yake ya awali.
Ni pendekezo ambalo kimsingi halina mantiki wala mashiko, na hatua ya Rais Donald Trump ya kuhamishia ubalozi wa Marekani kwenda Yerusalemu ni kielelezo kuwa uhalisia wa nchi ya Israel katika mipaka yake ya sasa ni suala ambalo halina ubishi tena.
Kama alivyoeleza Trump wakati akitangaza uamuzi huo, marais waliopita nchini Marekani walitoa ahadi za kuchukua hatua hiyo katika kampeni za uchaguzi ila wakasita, wakihofia dhahma kote duniani.
Uwezo wa Rais Trump kuchukua hatua hiyo ni mchanganyiko wa hulka yake binafsi na uelekeo wake kisiasa na kijamii, na kuchaguliwa kwake katika mazingira hayo kunatokana pia na hali halisi nchini Marekani kama inavyojijenga kutokana na uhalisia wa ushindani duniani.
Ni mazingira ambako kuna wasiwasi mkubwa kuhusu nafasi ya Marekani katika dunia kama viwanda vikubwa takriban vyote vinahamia China, halafu Marekani ibakie na viwanda tete vya teknohama, na kupokea fedha nyingi za uwekezaji (soko kubwa, huria, kodi ndogo, usiri wa mabenki, lugha ya Kiingereza, mchanganyiko wa mataifa, lugha na dini za aina zote duniani) iridhike na raha hiyo.
Nguvu za Marekani zinadhihirishwa na kinachotokea Mashariki ya Kati, ila isingewezekana kufikia hapo bila kuwepo serikali inayotokana na wasiwasi wa kina wa uwepo wa Marekani kama taifa kubwa, inayotaka ‘kuifanya Marekani kuu tena.’
Kushindwa kwa nchi za Kiarabu na nyinginezo za Kiislamu ambazo kwa jadi yao zimekuwa mahasimu wa Israel, tangu iundwe kwa kunyang’anya ardhi wenyeji waliokuwa eneo hilo (kipande kidogo cha eneo pana la Mashariki ya Kati ambako ardhi ya kuwapa waliohamishwa au kukimbia vita eneo hilo ingekuwa kazi rahisi katika mazingira tofauti) kuvunja uhusiano na Marekani kwa suala la ubalozi ndiyo mwisho wa kila kitu.
Endapo zingekuwa na uwezo zaidi hatua hiyo ingefuata, lakini kimsingi dunia nzima inajua suala la Yerusalemu lilishamalizika kuwa haitarudi au kugawanywa, lakini hali hiyo haikuwepo kisheria.
Ambacho hakiwezi kufanyika ni kugusa msikiti wa Al Aqsa, hata kama Israel itataka kujenga hekalu lake jipya la kihistoria, kwani la kwanza (la Mfalme Sulemani) na la pili (la nabii Ezra) yalijengwa hapo pia.
Ukiangalia kwa karibu unakuta kuwa kinachotokea sasa ndiyo uthibitisho wa kilichotabiriwa nchini Israel katika miaka ya karibuni, na mtu aliyekuwa kuhani mkuu aliyepita (ingawa hilo halionekani kwa urahisi katika mitandao, baadhi wakisema alikuwa tu kuhani).
Wakati anafariki kuhani huyo mwandamizi kabla ya mwaka 2014 kuanza, waziri mkuu wa zamani Ariel Sharon alikuwa bado anaendelea na ile ya kutokuwa na fahamu hospitalini, iliyodumu kwa miaka minane ndipo akafa – baada ya kuonekana akirudia fahamu kwa taabu, na kwa muda mfupi akiwa bado taabani.
Ni jambo lilitokea kwake mwaka 2005, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Palestina, Yassir Arafat, ambaye Sharon alikuwa naye kama mfungwa tu kwenye eneo la utawala la Mamlaka ya Palestina huko Ramallah, na bado akaagiza awekewe sumu na kufa, kinyume cha sheria zote za vita kimataifa.
Kwa vile malipo ni hapa hapa, haikupita muda, akaingia ‘comatose,’ yaani hali ya kuwa mgonjwa mahtuti anayekaribia kufa, na akabaki hivyo miaka minane – ambayo ina maana kuwa muda uliopangwa wa maisha yake ulifikiwa, ila alitumikia adhabu hiyo kwa kosa hilo kuu.
Wakati Sharon anafariki dunia (na kuhani alitabiri kuwa akifariki ndiyo masihi atakapofika), tayari kulikuwa na uasi mkubwa umeanza katika eneo la Mashariki ya Kati, kujumuishwa kwa vikundi vya wapiganaji wa Kisunni waliokuwa awali wanaunga mkono utawala wa hayati Saddam Hussein nchini Irak, wakaweka lengo kubwa zaidi (ya kile walichotakiwa kukifanya, na wafadhili wao wa Marekani na Uturuki, zaidi).
Wakapania kuunda ‘dola ya Kiislamu ya Iraq na Shamu,’ hiyo ya pili ikiwa na maana Syria na Lebanon pamoja, ikiwa ni moja ya matarajio ya baadhi ya mikondo ya fikra kuhusu ujio wa Madhi, anayeonekana kama mpambanaji anayekamilisha kufikia dola ya Kiislamu iliyokuweko kabla ya ufalme kuuondoa uhalifa.
Kumbe picha hiyo ina mikanganyiko yake, na kilichotokea ni udhihirishwaji wa Masih al Dajjal, nguvu ya uteketezaji inayoinuliwa katika umma wa Kiislamu, na siyo u-Mahdi halisi.
Vita hii ya makundi ya kuchinja yeyote asiyefuata mafundisho na sheria za dhehebu la u-Wahhabi nchini Saudia (ambalo sasa limeanza kubadilishwa kwa kina na ufalme mpya ulioko madarakani ambayo sasa unaendana na u-Mahdi, yaani kujumuika kwa Uislamu na Ukristo katika undugu, ilidhohofisha kwa kina nchi za Mashariki ya Kati.
Na bado kuna vita kubwa inaendelea nchini Yemen ambako Saudi Arabia na washirika wake wa Ghuba (ya Uajemi, ukitaka) wanapambana na ‘waasi’ wa ki-Houthi (labda ni ndugu wa waasi wa ki-Hutu) kwani nchi hiyo ina wa-Shia wengi zaidi lakini koo za ki-Sunni zinatawala, kama ilivyokuwa nchini Iraq, na kinyume chake ndiyo Syria. Wananchi wengi zaidi ni wa-Sunni, ila utawala ni wa Shia.
Udhaifu huu wa nchi za Mashariki ya Kati umetokana kwa upande mmoja na wimbi la demokrasia katika eneo hilo baada ya kuchaguliwa Barak Hussein Obama kuwa rais wa Marekani mwishoni mwa mwaka 2008, akafika Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri, akawaambia Marekani haiko vitani, na kamwe haitaingia vitani na Uislamu.
Wakamwamini, kwani yeye ni mwana wa Mwislamu kutoka Kenya. Endapo raia wa Marekani wangekuwa wanauchukia Uislamu, mzaliwa huyu wa Muislamu, au mtumwa (lugha ya zamani ya kibaguzi au dharau) kutoka Afrika, angeupata wapi urais nchini humo?
Hivyo, wananchi na hasa tabaka la wanafunzi kote Mashariki ya Kati wakaanza kutafuta demokrasia, siyo walindwe na madikteta dhidi ya Marekani na Uyahudi, wakajua ni kiini macho, na ni kwa maslahi yao wenyewe.
Ni kuukubali kwa dhati utandawazi, na hilo linawezesha Israel ichukue nafasi yake, na kuanguka kwa kudumu kwa bei ya petroli kutokana na Marekani kuzalisha petroli zaidi ya mshirika wake Saudia au Russia inazidi kubamiza nchi hizo, zisiwe na pa kutokeza Iran kujijenga Syria zikawa mavumbi, Israel ilipopiga ndege zote.
Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa
No comments
Post a Comment