DAWA YA ASILI YA FANGASI UKENI
Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa.
Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea:
1. LEMONADE
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
*Chukua asali mbichi nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.
*Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
*Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.
Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
2. MAZIWA YA MTINDI
Mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi, ni tiba ya kuaminika ya fangasi wa ukeni. Unaweza kutumia njia yeyeote kuweka maziwa ya mtindi au yogati kiasi kidogo labda kijiko kidogo cha chai ukeni wakati wa kulala na asubuhi unajisafisha kama kawaida.
Pia inashauriwa kula tu huu mtindi kiasi cha kutosha kila siku.
Uke wenyewe una uwezo wa kuondoa mabaki yote ya mtindi na kubakisha kiwango kikubwa cha bakteria wazuri (lactobacillus) pamoja na hali ya tindikali yenye uwezo wa kuzuia kujitokeza na kukua kwa fangasi. Bakteria hawa wanaopatikana katiaka mtindi hukusanywa viwandani na huuzwa kama bidhaa ijulikanayo kwa kitaalamu kama “Supplements of Acidophiles”.
3. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje
chukua punje 6
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na asubuhi ukiamka tu.
Fanya hivi kila siku kwa wiki 2 hadi tatu. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
4. MAFUTA YA NAZI
Kama fangasi hao wa ukeni wanajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na unapata muwasho pia, hakikisha unapakaa mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii dawa tosha kwa fangasi wowote juu ya ngozi.
MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:
Fangasi hii inaweza ikachelewa kupona au ikawa inajirudia hata baada ya kupona kama hutazingatia yafuatayo:
*Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
*Punguza vyakula vyenye wanga
*Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
*Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
*Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko
*Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
Ukiitaji dawa au ushauri
Dr Hamza
0654729438
0746025804
No comments
Post a Comment