Followers

JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???*


Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu wa *MEDICINE (Science)!!*
Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani  Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.
Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.
*FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU*
Kunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
Unapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
Nyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
Nyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
Nyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
Nyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini

*HASARA YA NYAMA YA NGURUWE*
Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
Nyama ya nguruwe ; ina sumu ya *carcinogen* ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani ( *WHO*), Na *The International Agency for Research on Cancer!!* Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
Anasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na *Centers for Disease Control and Prevention* inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi za *MAREKANI*
Nyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; *ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:*
✅Homa kali sana
✅Kichwa kuuma 
✅Kukosa nguvu 
✅Maumivu ya nyama za mwili
✅Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
✅Kuvimba uso Na kope 
✅Kudhuriwa Na mwanga 
Nyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
Wadudu wengine ni kama;
籠Nipah virus
籠Menangle virus
籠Viruses Ktk kundi Paramyxoviridae 
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
Nyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) Na *ANTIBIOTICS*
Nyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) - Reference....open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii. 
Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.

*JEE NG'OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??*
Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
Nani anaepika huku akipima joto limefika au laa???

*HITIMISHO*
Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!

*IMEANDIKWA NA ;*
Dr Isack
0715691898

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.