NJIA SITA (6) ZA KUEPUKA UMASIKINI
1. PATA MKE SAHIHI- Achana na wanawake Warembo ila Kichwani ni Zero. Pata mke ambaye sio tu ataunga mkono maono yako lakini pia atakusukuma ili uyafikie maono. Mwanamke atakaye kuvutia upambane sio kukukatisha tamaa. Apataye mke mwema apata kitu chema.
2. ACHA KUNYWA VINYWAJI VYA BEI RAHISI NA CHAKULA CHA BEI RAHISI - Sio tatizo kutoka out mara moja moja ukijumuika na Wenzako au wakati Unatengeneza Network ila Ujue unapokunywa Vinywaji vya rahisi au chakula cha bei rahisi maeneo rahisi unakutana na watu rahisi wasio na mawazo Makubwa na Pengine mawazo rahisi ya baadae. Nafasi kubwa za Kibiashra zinapatikana mahali ambapo Vinywaji ni ghali au chakula Ghali. Kwa iyo maeneo wanakouza Vinywaji au chakula rahisi aina ya watu utakaowakuta ni wale ambao watakuomba pesa au Uwanunulie. Pia wanaweza Kukufurahia kuwa mnunuzi mkubwa amefika, pata marafiki wazuri watakaokupa changamoto za kuendelea kimaisha, achana na marafiki wasio na faida yoyote.
3. ACHA UVIVU - Fanya kazi kwa Bidii sio Unalala sana kutwa umekaa tu kupiga majungu au Soga tena nyingine ni story za kuita watu wenye Maendeleo ni Freemason kila siku unalalamika. Usipoacha Uvivu umasikini Unakuotea.
4. TAMBUA VITU VINAVOZALISHA - Ukiwa na tabia ya Kuwaza hovyo Utakuwa na maisha ya hovyo. Kuna watu Ambao wako Vizuri sana kuzungumza habari za Wanaume au wanawake, mpira, Sinema, nani Tajiri nani masikini, kushindia kwenye mitandao ya kijamii watsap instagram au facebook wakati haingizi chochote mfukoni , nani hana au ana nini n.k lakini hazungumzii Uwekezaji, Ubunifu Biashara n.k hili haliiitaji elimu ya Chuo kikuu.
5. JIUNGE/KAA NA WATU WAKUBWA. Watu wengi hufeli kwa kuwa hawana watu Ambao wanaweza kujifunza kwao. Hata Simba ama Chui hujifunza kuwinda kwa wakubwa wao.. In short KAA NA WALE WALIONACHO, Usiishi kama MBUZI bila ratiba yoyote maisha ni kupanga na kuchagua, hata aliye mzee wa sasa jana alikua kijana kama ww, ukichezea ujana wako na muda wako wa sasa bdae usisumbue watu, Usipojipanga subiri maisha yatakupanga,
6. FANYA KAZI. Acha kupoteza Muda mrefu kushindia kanisani kusubiri Mazoezi ya kwaya au Kusali na Kufunga bila Kazi wakati Biblia imeagiza Mungu atabariki kazi ya Mikono yako. Baraka zitakufuata Wakati unafanya kitu. Usitumie Sala, mizunguko ya uimbaji ziara zisizokua na kikomo au mialiko mfululizo mwaka mzima kama kigezo cha Kutofanya Kazi kwa bidii au kujificha kwenye kichaka cha uinjilist bila kufanya kazi, kumbuka leo yako ndio hatima yako ya bdae,
No comments
Post a Comment