Diamond hizi stori za kukopi tumezichoka
Bill Shankly
DIAMOND Platnumz atabaki kuwa mwanamageuzi wa muziki wa Bongo Fleva, ataendelea kuwa msanii wa kwanza kuwekeza pesa nyingi na kupata mafanikio kwenye kiwanda cha muziki.
Nenda Kamwambie ndio rekodi yake ya kwanza kumtambulisha kwenye gemu, Number One remix aliyofanya na mkali Davido itabaki kuwa rekodi iliyofungua mipaka ya nje ya Nchi.
Tangu hapo ameendelea kuwa msanii mwenye mafanikio zaidi kwenye gemu ya Bongo Fleva, awards zaidi ya 22 huku akiwa nominated kwenye tuzo 28 zinamueka katika daraja la juu kabisa.
Sifa kubwa kwake ni namna ambavyo amefanikiwa kuwafungulia Dunia vijana wengi ambao anafanya nao kazi kwenye lebo yake ya Wasafi.
Rayvanny! Huyu ndie msanii pekee kutoka Bongo hadi Afrika Mashariki anaeshikilia rekodi ya kutwaa tuzo ya BET Award katika kipengele cha best viewers choice. Heshima hii imekuja akiwa chini ya WCB. Kwanini tusimpe heko Diamond?
Harmonize hakua na ndoto za kuwa hapa alipo leo, lakini toka akutane na Diamond usiku ule pale Dar Live kila kitu kimebadilika maishani mwake na leo anatajwa kama mmoja wa wasanii wenye nguvu kubwa Afrika Mashariki.
LIPO HILI LINALOKERA
Sampling kwenye muziki ni jambo la kawaida sana, kufanya refrix na cover pia sio vitu vigeni, tatizo ni pale tunapo-copy kiasi cha kugeuza kuwa mazoea.
Eneka yake Diamond Platnumz alifanya sample ya wimbo wa Fall wa Davido mbaya zaidi hadi maudhui ya video yalifanana, watu tukasema labda ni bahati mbaya (haha).
Ngoma ya picha yake ambayo imeimbwa na mkali mwingine kutoka Wasafini, Mbosso licha ya ukali wake lakini pia kuna baadhi ya shot ambazo zinafanana na wimbo wa R Kelly, When a woman loves.
Katika video hiyo kuna Scene Mbosso anaonekana akiwa na Micrphones nyingii sana huku akiwa amevalia suti hii ni copy kutoka kwenye video hiyo ya R.Kelly.
Wimbi la Diamond na lebo yake kuendelea kukopi video limeendelea tena kwenye moja ya ngoma yake mwenyewe iliyopo kwenye album yake ya A boy from Tandale.
Rekodi inaitwa Baila ambayo video yake imefanyikia Uingereza na asilimia 90 imekuwa copy&paste kutoka kwenye wimbo wa mkali Sharukh Khan uitwao Jab Tak Hai Jaan ambao umetumika kwenye movie ya Saans.
Copy and paste ya wimbo huu ulizua mjadala maana kila kitu kilikua ni sawa kuanzia, location, shots na scenes. Kila ambacho kilifanywa na Sharukh basi Diamond amekifanya kwenye Baila.
Baadaye akaja na 'utetezi' dhaifu eti video imeonesha jinsi gani Sharukh ni role model wake ingawa kwenye ile list ya watu 14 ambao wamemu-inspire Mdosi hayupo.
WASAFI HAWAJAKOMA
Licha ya watu kuzidi kumshambulia Diamond na team yake kwa namna ambavyo wanacopy bado tena jana wamerudia kile kile.
Rekodi mpya ya mkali Lavalava iitwayo, Gundu iliyotoka jana imerudia 'makosa' yaleyale.
Video ya Gundu kwa asilimia 75 inafanana na video ya Bambi yake Supastaa, Jidena kutokea mandishi matatu USA.
Namna ambavyo Jidenna anaonekana kukimbia barabarani akiwa amevalia suti yake ya cream na simple nyeupe chini huku akionekana kupishana na watu wakifanya jogging na wengine wakiendesha baiskeli ndivyo ilivyokuwa kwenye video ya Lavalava.
Hili sasa limegeuka kuwa tatizo, lebo kubwa kama ya Wasafi haiwezi kuwa kila siku inaingia kwenye shutuma za kukopi video za wengine.
Ingependeza kama wao ndio wangekuwa wanakopiwa video zao kwa status aliyonayo Diamond na team yake.
Maswali ya kujiuliza wanapanga kufanya video hizo kwa kukopi au ma-Director ndo huwaingizaga chaka?
Na kama wakimrushia lawama director pia litakua jambo la kushangaza kuona lebo kubwa kama WCB haina watalaamu wa video analysis.
Lakini lipo lile linalosemwa kwamba Diamond amekuwa akiingilia majukumu ya ma-director wengi, kwamba muda mwingine anakuja na idea/script zake mwenyewe.
Huku kuendelea kucopy video kwa staili hii kunaidhoofisha afya ya Diamond mwenyewe na lebo yake, itafikia hatua watakuwa wakiachia video hakuna ambaye atashtuka maana tutakua hatutegemei kitu kipya.
Kama unamkubali mtu basi na ni role model wako basi ngoma ifanyie cover au refrix na isitoke kibiashara, on top of that isiwe mazoea kama ambavyo WCB wameamua kuishi kwa kutegemea creativity ya watu wengine
Ambacho hajui anazidi kuwaweka pabaya mashabiki wake mbele ya team ya mpinzani wake mkubwa kwenye game, watu sasa hivi wanachukua pointi za bure kwa 'ujinga' wa kukopi na kupesti. Aibu!
Salamu hizi zisimuendee Richard Messi Mavoko.
0683 015145
No comments
Post a Comment