BREAKING: VIDEO: Sakata la Makontena ya Makonda latua kwa Rais Magufuli, Aamuru Haya
Kwa mara ya kwanza Rais John Magufuli ameliongelea sakata la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda yaliyozuiliwa bandarini na TRA yakitakiwa kulipiwa ushuru kama ambavyo sheria inaelekeza.
" Ni mtu mmoja pekee nchini ambaye amepewa dhamana kwa kujibu wa sheria ya fedha, madeni, sheria ya dhamana na misaada kupitia sheria namba 30 ya mwaka 1974 kifungu cha (3), (6), (13), (15) ndiye amepewa dhamana ya kupokea misaada kwa niaba ya Nchi hakuna mtu mwingine, hayupo.
" Sasa ukichukua makontena kule umezungumza sijui na watu wengine au na wafanyabiashara unasema una makontena yako halafu unasema ni ya waalimu, wala hata shule hazitajwi, maana yake nini? maana yake siunataka utumie walimu? ulete hayo makontena upeleke shule mbili tatu ndizo zitapewa mengine utakwenda kuyauza upeleke kwenye shopping mall kwahiyo wafanyakazi wasitumike kwa maslahi ya watu fulani," amesema Rais Magufuli.
No comments
Post a Comment