Diamond, Mavoko wakutanishwa na Basata leo, Wagoma kuongea
MSANII wa Bongo Fleva, Rich Mavoko na uongozi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond Platnumz na Sallam SK, wamekutana tena kwenye ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa lengo la majadiliano baada ya Mavoko kulalamikia kile alichodai ni mkataba wa unyonyaji aliosainishwa na WCB.
Pamoja na kukutana, pande zote hazikuweka wazi kilichokuwa kinaendelea.
Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 na alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo kwa madai ya kunyonywa kimaslahi.
Katika hali ya kushangaza Mavoko aligeuka mbogo mbele ya wandishi wa habari waliotaka kufahamu nini kilichojiri kwenye kikao, " Unataka nizungumze nini? wewe ni nani? unanilipa nikiongea?" Mavoko huyo akiwajibu wandishi.
Katibu wa Basata, Godfrey Mngereza amesema wamefanya mazungumzo na wasanii hao na kwamba hakuna tatizo lolote baina yao huku akisema wamekubaliana katika yale yaliyokuwa yakijadiliwa ingwa mengine ni ya ndani hawezi kuyaweka wazi
Aidha, alidaiwa kuna vitu ndani ya mkataba huo hakutimiziwa na mabosi wake kama mkataba ulivyokuwa ukielekeza.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya, Meneja wa Diamond, Salam SK, hivi karibuni na kituo kimoja cha redio hapa nchini alipoulizwa kuhusiana na madai haya ya Mavoko alisema; “Mavoko bado ni msanii wa WCB na hayo malalamiko anayotoa sisi hatujui yanahusiana na nini kwani huduma zote wanazopatiwa wasanii wa WCB anazipata”.
“Kabla ya Mavoko kusaini mkataba alipewa akakae nao aupitie hadi ajiridhishe na Mavoko alifanya hivyo. Alikaa nao ndani kwa muda wa wiki mbili na mwisho wa siku akasaini mwenyewe, sasa anacholalamika ni nini? Mkataba huo una kurasa kumi, kwa hiyo sisi hatujui ni kitu gani anataka haswa,” alisema Salam.
Baada ya Mavoko kupeleka malalamiko hayo Basata, waliamua kuwaita viongozi wake wa WCB walipofika wakaongea nao na ndipo wakakubaliana wakutane BASATA leo Augosti 23.
No comments
Post a Comment