Viwango vya huduma katika bandari ya Mtwara vyaongezeka
Biashara na viwango vya huduma katika Bandari ya Mtwara vimeongezeka baada ya serikali kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika bandari hiyo ambapo kiwango cha mizigo inayosafirishwa nje ya nchi kimeongezeka kutoka tani lakimbili mwaka 2015 hadi tani laki tatu na elfu sitini na tano mwaka 2017.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Bwana Abdulah Salim wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango, alipotembelea na kukagua utendaji kazi wa Bandari hiyo ambayo pia imeanza kupokea shehena ya mafuta.
Aidha, amesema kiwango cha mizigo inayosafirishwa kupitia Bandari hiyo kinatarajia kuongezeka zaidi aada ya serikali kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mia moja arobaini , kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo ili iweze kuhudumia meli nyingi na kubwa kutoka pembe zote za dunia.
Waziri Mpango amesema serikali imeamua kuwekeza fedha nyingi katika Bandari ya Mtwara, ili iweze kusaidia nchi kuingiza mapato kwa njia ya kodi na ushuru kutokana na uwepo wa nchi nyingi jirani ikiwemo Msumbiji, ambazo zitatumia bandari hiyo kusafirisha mizigo yao na hivyo kukuza pia uchumi wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
No comments
Post a Comment