Followers

Shilole awachimba mkwara mzito wanaume

 


Msanii wa BongoFleva na mjasiriamali nchini Tanzania, Zuwena Mohamed maarufu kama 'Shishi Babe', amewaonya wanaume wote kuacha tabia ya kuwaona wanawake kama chombo cha starehe, na badala yake amewataka waishi kiakili na wanawake zao kusudi waweze kuvushana kwenye mafanikio yao.

Shilole ametoa onyo hilo kupitia ukurasa wake wa kijamii mchana wa leo Agosti 31, 2018, baada ya kuwepo wimbi kubwa la wanaume hususani waliopo kwenye ndoa au mahusiano ya kimapenzi, kutowaheshimu wanawake kutokana na maumbile yao huku wengine wakijisahau kuwa hakuna mafanikio yoyote bila ya uwepo wa wanawake hao.

"Sio kila mwanamke unayemuona ni chombo cha starehe, wengine ni ufunguo wa mafanikio yako. Heshima kwa wanaume wote wanaoheshimu wanawake", ameandika Shilole.

Katika baadhi ya jamii kumekuwepo na vijitabia vidogo vidogo ambavyo hupelekea kumchukulia mtoto wa kike kutokuwa na thamani, kwa kile wanachokiamini kuwa mwanawake ameumbwa kwa lengo la kuwapa starehe tu hapa duniani nasio kutoa changamoto katika kujiendelea kiuchumi uchumi wa maisha na kutaka kula starehe peke yake bila ya kujali kesho yao.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.