Followers

CCM yawabwaga wapinzani Ubunge Liwale, Kuchauka ashinda kwa kishindo



Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge

Msimamizi uchaguzi Jimboni hapo Luiza Mlelwa amesema waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405

Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81.Mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge, Kuchauka amesema ameyapokea matokeo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zilizopo

Aidha Kuchauka amesema changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwaleni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, Elimu, mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo.

Abdul Kombo Ngakolwa mgombea wa chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa(CCM) na amempongeza, kwa ushindi huo '' Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani'' alisema Abdul

Mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vifuatavyo AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT 285 sawa 0.79%CUF 5207 sawa na 12. 92%.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.