Followers

Hemedy PhD atangaza umri wa kuoa

Msanii wa Filamu Bongo, Hemedy PhD amesema kuwa ataoa atakapofikisha umri wa miaka 45.

Muigizaji huyo amesema hayo kwenye mahojiano na SnS Tanzania ambapo ameeleza yeye na mpenzi wake ndivyo walivyokubaliana.

"Mimi nimepanga nitaoa nikiwa na umri wa miaka 45 ili nitaoa ila nina mpenzi wangu ambaye ninampenda na ninaamini nitafika naye, kwa hiyo kaamua kunichagua, kaamua kunivumilia," amesema Hemedy.

Katika hatua nyingine Hemedy ameeleza kuwa siku si nyingi ataachia wimbo wake mpya mara baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kuaandaa tamthilia. 

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.