Fahamu huduma ya kwanza kwa mgonjwa anayetokwa damu puani
Tatizo la kutokwa na damu puani husababishwa na kupasuka kwa mishipa midogomidogo inayosambaza damu puani. Tatizo hili hutokea kwenye tundu moja ama yote ya pua na linaweza kusababisha hata kifo kama halitapatiwa ufumbuzi kwa muda muafaka.
Nini sababu za kutokwa na damu puani?
Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha mtu kutokwa na damu puani na miongoni mwa hizo sababu ni;
Kupasuka kwa mirija ya damu inayopeleka damu kwenye maeneo ya pua.Shinikizo la damu kuongezeka (High blood pressure)Kupiga chafya (sneezing)Kupenga kwa nguvu.
Jinsi ya kutoa huduma kwa mtu anayetokwa damu puani.
Mruhusu mginjwa akae. (Usimlaze chali maana damu inaweza kurudi na kuziba mirija ya hewa na mgonjwa akashindwa kupumua)Hakikisha milango ya hewa (Mdomo) iko wazi ili mgonjwa aendelee kupata hewa safi ya Oksijeni.Mkalishe akiwa ameinama kidogo kuelekea mbele.Binya kidogo matundu ya pua yake kwa muda kidogo. (Mgonjwa mwenyewe anaweza kufanya hivi pia kama hajazidiwa sana)Mwambie avute hewa kupitia mdomo na siyo pua maana utakuwa umeiziba.Baada ya muda kidogo achia halafu uangalie kama damu imeacha kutoka.Endelea kwa utaratibu huu (wa kubinya pua na kuachia baada ya muda) kama mara nyingi.Kama damu haijaacha kutoka kwa muda wa dakika 30, basi MWAHISHE MGONJWA WAKO HOSPITALI kwa matibabu zaidi
ZINGATIA
Kama mtu anatokwa damu puani, lengo lako kubwa la kumsaidia ni kuhakikisha unaondoa au unapunguza tatizo la damu kuendelea kutoka kwa mtu huyu.
Wakati unaendelea kumsaidia mgonjwa, mwambie azingatie haya;
Asiongee.Ajizuie kukohoa.Asiteme mate.
Kumzuia mgonjwa kufanya niliyokueleza hapo juu ni ili kuzuia kuharibu mabongemabonge ya damu ambayo yanaweza kuwa yamejitengeneza puani na kusababisha damu ziendelee kutoka
No comments
Post a Comment