Followers

Hizi ndio hatua 10 za kuanzisha bustani ya nyumbani ( home garden)


Kabla ya kuziangalia hizi hatua 10 za kuanzisha bustani yako nyumbani ni vyema tukaweza kujua umuhimu wa bustani ya nyumbani.

Baadhi ya umuhimu wa bustani ya nyumbani ni pamoja na:
1. Kupata hewa safi na ya asili
2. Kupata sehemu nzuri ya kupumzikia nje ya nyumba.
3. Kupendezesha muonekano wa nje wa nyumba yako.
4. Kupangilia na kuainisha matumizi ya ardhi ya nje.

HATUA 10 ZA KUANZISHA BUSTANI YA NYUMBANI

1. WAZO:
Je itakuwa ni bustani ya maua? majani? au mboga mboga?.
Kama itakuwa ni maua je ya aina gani? aidha ni maua ya kudumu (Perennial Flowers) ambayo hustawi kwa muda mfupi lakini yanauwezo wa kustawi tena na tena kwa kila mwaka. au unafikiria maua ya muda mfupi ( annual flowers) ambayo utahitajika kuyapanda tena na tena katika mwaka mmoja lakini hustawi vizuri sana na kuipa nyumba yako muonekano mzuri.

Lakini unaweza ukaamua kupanda aina fulani ya maua kisha ukabadili kwa aina nyingine punde tu utakapo kufanya hivyo.

2. CHAGUA SEHEMU:
Maua yote na mboga mboga uhitaji takribani saa 6 za jua kamili kwa kila siku.
Hivyo tumia angalau siku moja kuchunguza jinsi jua linavyopita katika sehemu uliyoichagua kuanzisha bustani yako.

Kama sehemu yako haipati jua sana kwa siku ni vyema kuonana na mtaalamu ambaye atakushauri ni maua ya aina gani au mbogamboga zipi zitafaa kwa eneo lako.
Ni vizuri kuchagua eneo ambalo lipo karibu na chanzo cha maji au katika sehemu ambayo unapendelea kutumia muda wako kukaa na sehemu ambayo itakuruhusu kutazama vivutio vilivyopo karibu na nyumba yako.

3. SAFISHA ARDHI:
Ondoa tabaka la ardhi ambalo lina uoto ambao huuhitaji katika eneo lako pendekezwa kisha safisha eneo lako vizuri.

4. BORESHA UDONGO:
Kama ardhi yako haina rutuba, ni vizuri ukaongeza thamani yake kwa kuongeza mbolea au tabaka la mchanganyiko wa nyasi zilizooza katika sehemu yako.

5. LIMA:
Ili kuweza kuruhusu maji kupenya kwa urahisi, lima sehemu ya ardhi yako pendekezwa.
Kabla ya Kulima hakikisha ardhi yako ina maji maji kiasi, Tafadhali sana usilime katika ardhi ambayo imekauka sana na wala ambayo ina maji maji sana kwasababu kulima kwako kutapelekea kuharibu mshikano mzuri wa udongo wa eneo lako pendekezwa.

Kwa bustani ya maua ni vyema kulima mara moja tu kwa mwaka kabla ya kupanda kipindi cha majira ya kuchipua. Tunapendekeza kuonana na mtaalam kabla ya kuanza mchakato ili aweze kutambua aina ya udongo wa sehemu yako na kukupa ushauri wa kina.

6. PATA MICHE:
Unaweza kwenda sehemu zenye vituo vya bustani na kununua miche yako pia kumbuka kuhagua mimea inayoendana na hali ya hewa ya eneo ulilopo na aina ya udongo wa sehemu yako ulipo.

7. PANDA MICHE:
Kuna baadhi ya miche inastawi zaidi kipindi cha joto au baridi ,hivyo ni vizuri kusoma maelezo vizuri ya mbegu au miche uliyopewa kabla ya kupanda ili uweze kubaini ni wakati upi ni muafaka kwa wewe kuanza kupanda.

8. MWAGILIA:
Miche haipaswi kukauka,mwagilia kila siku pindi angali midogo midogo hadi mizizi yake itapochipua. Baada ya hapo umwagiliaji utategemea na aina ya udongo wa eneo lako, na hali ya hewa ya eneo lako na kiasi cha mvua.

9. PALILIA:

Mara kwa mara ondoa magugu ili bustani yako iweze kustawi vizuri. Kumbuka magugu yakiwa mengi yataharibu muonekano wa bustani yako na kuondoa mvuto.

10. MATUNZO:

Bustani yako tayari ipo kwenye mstari sahihi, zidisha bidii kupalilia na kumwagilia.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.