Kocha Azam FC ajipa matumaini kuifikia nafasi ya Yanga SC
Kocha wa Azam FC Hans Pluijm amejipa matumaini ya kuwa nafasi ya kwanza iliyo mikononi mwa Yanga baada ya kufikisha pointi 47 wakiwa wamecheza michezo 20 sawa na Yanga ambao wana Pointi 53 wakiwa nafasi ya kwanza
Kocha huyo amesema kikosi chake kinacheza kwa hesabu kali hali inayofanya kipate matokeo katika michezo yake hivyo ni suala la wakati kushika nafasi ya kwanza.
"Kwenye mpira kila kitu kinawezekana kikubwa ni mipango na hesabu, hakuna haja ya kuwa na hofu kama una kikosi kizuri na kinapata matokeo suala la nafasi ni muda tu.
Hata hivyo amesema Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo hivyo ni wakati wao kutafuta matokeo kwa nidhamu wakiwa ndani ya Uwanja kupitia hayo wataushangaza ulimwengu wa mpira kama ilivyo kwa sasa
No comments
Post a Comment