Followers

Matengenezo ya Bararara Mkoani Pwani kutumia bil. 25.4



Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoani Pwani Yudas Msangi, amesema mkoa huo unatarajia kutumia kiasi cha sh.bilioni 25.4 kwa ajili ya kufanya matengenezo mbalimbali ya barabara kwa bajeti ya mwaka 2018-2019.

Mhandisi huyo ameyasema hayo wakati wa kikao cha bodi ya barabara cha mkoa huo na kusema kuwa hadi kufikia septemba 2018 zimepokelewa kiasi cha sh. milioni 958.7  kwa ajili ya matengenezo mbalimbali.

“Katika kipindi hicho kiasi cha shilingi bilioni 2 zimetumika kufanya matengenezo mbalimbali kwenye barabara kuu”,

“Kazi za matengenezo zilichelewa kuanza kutokana na taratibu za manunuzi na uhakiki wa mikataba ambavyo huchukua muda mrefu kukamilika hasa mikataba inayohakikiwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali”alisema Msangi.

Pia Msangi alibainisha, mkoa umepanga kufanya miradi ya maendeleo ya barabara zenye urefu wa kilometa 32.5 zenye thamani ya sh.bilioni 2.3.

Alisema,meneja huyo alisema kwenye miradi hiyo ya maendeleo sh. bilioni 1.3 ni bajeti ambapo sh.milioni 969 ni kutoka mfuko wa barabara vilevile bilioni 7.5 ni kutoka serikali zitafanya ukarabati kwa kiwango cha changarawe/udongo.

Nae mkuu wa  mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza, ili kuboresha barabara za mkoa huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.