Simba SC imetinga robo fainali ya CAF Champions League
Club ya wekundu wa Msimbazi Simba SC leo March 16 2019 imeingia tena katika vitabu vya kihistoria baada ya kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya CAF Champions League, hiyo ni baada ya kumalizika kwa game yao mwisho ya Kundi D dhidi ya AS Vita.
Leo Simba SC ilikuwa nyumbani uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya AS Vita, ambapo Simba ikiwa nyumbani ilikuwa inahitaji ushindi pekee ndio ungewapa point za kusonga, Cloutous Chama dakika ya 90 ya mchezo amefunga goli la ushindi na kuipeleka Simba robo fainali.
Simba imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, licha ya AS Vita kupata goli la uongozi dakika ya 12, Simba SC ilifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mohamed Hussein dakika ya 35, ushindi huo sasa umeifanya Simba na Al Ahly kufuzu hatua ya robo fainali na AS Vita na JS Saoura kuaga mashindano hayo baada ya kumaliza nafasi ya tatu na nne.
Hata hivyo hilo linakuwa pigo kwa AS Vita kuondolewa hatua za mapema katika michuano hiyo, kwani ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kusinga mbele kutokana na msimu uliopita kufikia hatua ya fainaili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, timu za TP Mazembe, Esperance, Horoya, Simba SC, Al Ahly, Costantine, Mamelod Sundowns na Wydad Athletic Club ndio zimefuzu kucheza robo fainali.
No comments
Post a Comment