Daniel Arap Alazimika Kulipa Faaini Kwa Kunyakuwa Ardhi
Bwana moi alinyakua ardhi hiyo kinyume cha sheria miaka 36 iliyopita, lakini ilisajiliwa kwa jina la Bwana Moi mwaka 2007.
Mume wake Chelugui Noah Chelugui alikuwa chifu wakati wa utawala wa Bwana Moi.
Rais huyo wa zamani ambaye ndiye rais aliyekuwa mamlakani kwa muda mrefu zaidi , alishutumiwa na Bi Chelugui na mtoto wake wa kiume David Chelugui kwa kusajili ardhi ya familia yao kwa jina lake miaka miwili baada ya Bwana yake Bi Chelugui kufariki dunia.
Inasemekana baadae Bwana Moi aliiuza ardhi hiyo kwa kampuni ya utengenezaji wa mbao Plywood Limited.
Kampuni ya Rai Plywood Limited iliwaeleza majaji kuwa ilinunua ardhi hiyo kutoka kwa Moi mnamo mwaka 2007 baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa kisheria kuhusu ardhi hiyo.
Hata hivyo, Bwana Moi hakuweza kuipatia mahakama ushahidi wowote juu ya jinsi alivyopata ardhi, anasema mwandishi wa BBC Mercy Juma aliyepo Nairobi.
Jaji Anthony Ombwayo alisema Bwana Moi alikuwa na mienendo ya "isiyo ya kawaida, ukiukaji katiba, kutofuata utaratibu " na "yenye dosari ".
Bwana Moi alikuwa rais wa pili wa Kenya mwaka 1978 ambapo alihudumu hadi mwaka 2002.
Alilitawala taifa hilo kwa mkono wa chuma na alishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Kutokana na shinikizo la kimataifa, aliruhusu uchaguzi wa vyama vingi mnamo mwaka 1992 ,uliotawaliwa na ghasia zilizosambaa nchini na madai ya wizi wa kura.
Uamuzi wa kesi ni muhimu kwa Kenya.
Kumekuwa na kesi nyingi za unyakuzi wa ardhi unaodaiwa kufanywa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali na wafanyabiashara matajiri kwa miaka mingi, lakini waathiriwa hawana utashi wala pesa za kukabiliana na wanyakuzi.
Ufisadi katika mfumo wa mahakama ni tatizo jingine kubwa. Wakati mzozo unapopelekwa mahakamani, kesi huzoroteshwa kwa miaka mingi.
Wengi wanamatumaini kuwa hukumu hii dhidi ya Bwana Moi itaonekana kama jaribio na kwamba itatuma ujumbe kwa watu kwamba hawawezi tu kuwa wananyakua ardhi tena za watu maskini
No comments
Post a Comment