Mawandaz: Tafadhari soma kisa hiki ili ujifunze kitu
TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA SUPERNIDA BLOG,TUPIGIE SIMU 0767673288 AU 0675830390 Au kwa Barua pepe danielothmary@gmail.com Karibu
2, 2018 3:00 PM
Tafadhali soma kwa makini.
Hii stori imetokea kwenye familia ya kipato cha kati (kawaida).
Kijana hakupenda kuishi nyumbani kwao. Kwa sababu baba yake alikuwa anamsema kila Mara kwa usumbufu, ' unaacha chumba bila kuzima feni'
'TV haijazimwa,
'Weka peni vizuri'
Kijana hakupenda baba yake amseme kwa mambo madogo madogo kila Mara. Alivumilia kila siku alizokuwa anakaa pale nyumbani.
Lakini leo, amepata kuitwa kwenye usaili wa kazi. 'Hivi punde nitapata kazi, nitahama hapa nyumbani, Hakutakuwa na masemango tena ya baba' yalikuwa mawazo ya kijana.
Akiwa anajiandaa kuondoka kwenda kwenye usaili, baba akamwambia: ' Jibu maswali utakayopewa bila kusita. Hata kama haujui majibu, sema huku ukijiamini'. Akampa pesa zaidi ya zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya usaili.
Kijana alikifika kwenye usaili. Akaona hamna mlinzi getini. Geti lilikuwa wazi, kitasa kilikuwa hakijafungwa kikawa kinawakwaruza wanaopita. Akaweka kitasa vizuri akafunga geti akaingia ndani.
Njiani akaona maua yamepandwa vizuri. Mtunza bustani hakuwepo na hakufunga bomba, maji yakawa yanamwagika mpaka njiani. Akachukua mpira wa maji akaweka kwenye maua akaendelea na safari.
Mapokezi hapakuwa na mtu, kulikuwa na karatasi inasema usaili upo ghorofa ya kwanza. Taratibu akapanda ngazi.
Taa zilizowashwa usiku zilikuwa zinawaka bado mpaka ile saa nne asubuhi. Akakumbuka baba yake alivyokuwa anamkoromea, ' kwanini umeacha taa bila kuzima chumban?' Akahisi bado anasikia ile sauti. Ingawa alichukia vile alivyokumbuka, ila akazima zile taa.
Alipofika ghorofani akaona watu wengine nao wamefika wamekaa wanasubiri kuingia kwenye usaili. Aliangalia idadi ya namba ya watu ilivyokubwa akawaza kama kuna uwezekano wa kupata kazi.
Akawa anaingia kwa hofu akakanyaga zuria limeandikwa ' Karibu'. Alipoliangalia vizuri akagundua limewekwa chini juu juu chini. Akaliweka sawa lile zuria.
Akaona mistari mbele watu wengi wakisubiri zamu zao, ila nyuma nafasi ilikuwa tupu, lakini feni zilikuwa zikizunguka.
Akasikia sauti ya baba yake tena, ' kwanini umeacha feni inazunguka chumban?' Akazima feni ambazo zilikuwa hamna watu chini yake akakaa kwenye kiti.
Akaona watu wengi wanaingia kwenye chumba cha usaili na wanondoka muda mfupi tu kwa mlango mwingine. Kulikuwa hamna namna unaweza kujua nini kilikuwa kinaulizwa kwenye usaili.
Ilipofika zamu yake akaingia akasimama mbele kwa hofu.
Afisa akachukua vyeti vyake akamuuliza, ' lini utaanza kazi?'.
Akajiuliza, 'hili ni swali la mtego kwenye usaili au hii ni ishara nimepata kazi?" Alichanganyikiwa.
' Unawaza nini?" Boss akauliza. 'Hatukumuuliza yeyote yule maswali hapa. Kwa kuuliza maswali machache hatutaweza kufahamu uwezo wa yeyote. Hivyo jaribio lilikuwa ni kuangalia mwenendo wa mtu. Tuliweka majaribio kadhaa juu ya tabia ya mtu, na tukawa tunamuangalia kila mmoja kupitia CCTV. Hakuna hata mmoja aliyekuja Leo na kurekebisha komeo, mpira wa maji, zuria mlangoni, feni na taa za umeme. Wewe peke yako ndiye uliyefanya hayo. Ndio maana tumeamua kukuchagua wewe kwenye hii kazi', alisema boss.
......….............................
Alikuwa anakasirika alipokua anaelekezwa na baba yake. Sasa amefahamu kwamba ni yale maelekezo ndiyo yaliyompatia kazi. Hasira na chuki kwa baba yake zilipotea hapo hapo kabisa. Akaamua atamleta baba yake anapofanyia kazi na akaenda nyumbani kwa furaha.
Chochote baba zetu wanachotuambia ni kwa manufaa yetu wanadhamiria kutupatia maisha nzuri baadae.
Dhahabu haing'ai kama haitapitishwa kwenye moto.
Kwa sisi kuwa watu wazuri na kuwa na ustaarabu tunatakiwa tukubali kujishusha ili kuondoa tabia mbaya na mienendo mibaya ndani yetu. Hivyo ndivyo baba zetu wanafanya wanapotuadabisha.
Mama anambeba mtoto tumboni, anamyonyesha na anambeba. Lakini kwa baba haiko hivyo. Anamlea mtoto kwenye misingi stahiki ili afike mbali kuliko yeye alipofika.
Tunaelewa maumivu ya mama anayoyapitia kwa kumsikiliza, lakini maumivu ya baba tunayaelewa tukiambiwagwa na wengine tu.
Baba zetu ni waalimu wetu tukiwa wadogo, ila ni adui zetu tukifikisha umri wa miaka ishirini na wanakuwa mwangozo wetu kwa kipindi chote anachoishi.....
Mama anaweza kwenda kwa watoto wake kukaa lakini baba hawezi kufanya hivyo....
Hamna haja ya kuumiza wazazi wetu wakiwa hai na kuwakumbuka wakishafariki. Tuwajali na kuwasikiliza muda wote wa maisha yao.
Huu ni mfano kwa ajili ya mafunzo.
*TAFADHALI! sambaza kwa wazazi na watoto.
No comments
Post a Comment