Askari anayedaiwa kumuua mdogo wa Heche kizimbani tena
Tarime. Askari polisi E.1156 William Marwa leo Mei 15, 2018 amefikishwa kwa mara ya pili mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Tarime, akikabiliwa na shtaka la mauaji ya Suguta Chacha ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.
Kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Aprili 30, 2018 na kusomewa kesi ya mauaji namba, P176/2018 mbele ya Hakimu A.R. Kahimba.
Askari huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 27, 2018, amefikishwa mahakamani hapo leo asubuhi na gari ya polisi chini ya ulinzi mkali, akiwa sambamba na mahabusu wengine.
No comments
Post a Comment