China yapinga uchokozi wa Marekani kwenye bahari yake
TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA SUPERNIDA BLOG,KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIE SIMU 0767673288AU 0675830390
China imepinga vikali manowari mbili za Marekani kuingia kwenye eneo la bahari ya China karibu na Visiwa vya Xisha.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema manowari za Marekani ziliingia jana usiku kwenye eneo la bahari ya China karibu na Visiwa vya Xisha bila ruhusa ya serikali ya China. Jeshi la majini la China lilizitambua, kuzionya na kuzifukuza.
Bw. Lu Kang amesema visiwa vya Xisha siku zote ni ardhi ya China, na serikali ya China ilitangaza mpaka wa eneo la majini la Visiwa vya Xisha mwaka 1996.
Pia amesema kitendo hicho cha manowari za Marekani, kimekwenda kinyume cha sheria za China na za kimataifa, na kimeingilia vikali mamlaka ya China, na kuhatarisha amani, usalama na utaratibu kwenye maeneo husika ya bahari.
Pia amesisitiza kuwa China itachukua hatua zote za lazima kulinda mamlaka na usalama wake. Wizara ya Ulinzi ya China pia imepinga vikali kitendo hicho cha Marekani.
PAKUA[DOWNLOAD] SASA APPLICATION YA SUPERNIDA KUPATA HABARI ZOTE KILA SAA BONYEZA HAPA >>>>DOWNLOAD SASA BONYEZA HAPA.>>>>>
No comments
Post a Comment