Followers

Mbatia amshauri Rais Magufuli



Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia amefunguka na kuikumbusha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli juu ya adhma ya kujenga chuo cha kitaifa cha kisiasa nchini kitakachoweza kuwaanda viongozi wa kisiasa bila ya kujali itikadi za vyama vyao.

James Mbatia ametoa kauli leo Mei 07, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akiuliza swali kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusiana na makubaliano yaliyofanywa mwaka 2002-2004 kipindi cha serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa chini ya Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa.

Kutoka na hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amekubaliana na ombi hilo na kusema kupitia chuo hicho wanaamini wataweza kupata viongozi waliokuwa bora.

"Nia na dhamira ya serikali  ni kuendelea kukuza demokrasia ndani ya nchi na makubaliano yaliyofanyika mwaka 2002-2004 tutaendelea kuyafanyia kazi na kufuatilia ili ombi hili liweze kutimia la kuwa na chuo cha kuwaweka wanasiasa. Tunaamini kupitia chuo hicho basi tutakuwa tumejenga taifa la watu wazalendo na wenye ari ya kweli ya kuwatumikia watanzania", amesema Mavunde.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Antony Mavunde amesema sio kweli kwamba serikali inazuia harakati za kisiasa kufanyika nchini bali vyama hivyo kuna masharti maalum ya kufanya pidi wanapotaka kufanya mikutao yao.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.