ZIJUE DAWA ZA ASILI KWA KUKU
DAWA ZA ASILI KWA KUKU
Madawa ya Asili yatokanayo na Mimea yanayosaidia katika Tiba na Kinga za Maradhi mbalimbali ya Kuku . Sehemu za mimea zinaweza kuwa: Majani, Magome, Mbegu, Maua au Matunda .
Umuhimu wa kutumia tiba zenye asili ya mimea:
• Hupatikana kwa urahisi.
• Ni rahisi kutumia.
• Gharama nafuu.
• Zinatibu vizuri zikitumika vizuri
• Hazina madhara.
C. Baadhi ya Mimea inayotibu Maradhi ya Kuku:
1. Mwarobaini (Majani, Mizizi, Magome):
Hutibu magonjwa yafuatayo:
• Typhoid.
• Kuzuia Kideri.
• Kuhara.
• Mafua.
• Vidonda.
2. Shubiri Mwitu (Aloe vera):
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.
Mchanganyiko huu unaweza kutibu: • Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga. • Homa ya matumbo (Typhoid). • Mafua (Coryza). • Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
3. Mtakalang’onyo (Euphorbia):
Chukua Majani makubwa 3-5, ponda, weka katika lita 10 za maji kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mtakalang’onyo hutibu:
• Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba)
• Ndui. • Kuhara damu (Coccidiosis).
4. Mbarika (Nyonyo):
Hutibu Uvimbe. Weka majani ya mbarika ndani ya majani ya mgomba kisha weka ndani ya jivu la moto, kisha kanda sehemu yenye uvimbe kwa kutumia majani hayo ya mbarika.
5. Mlonge (Mlonje):
Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu: • Mafua. • Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga • Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). • Homa ya matumbo • Ini.
6. Konfrei:
• Ina madini na vitamini nyingi. • Hutibu vidonda na majipu.
7. Ndulele (Dungurusi, Makonde, Tura/Ndula):
• Majani hutibu Minyoo. • Matunda hutibu Vidonda.
8. Papai (Majani):
Cahemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1. Poza kisha chuja. Hutibu: Minyoo
Pia Majani Ya Mpapai Ni Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote
Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi.
- Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
Kutumia (kama kinga) - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia - Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. - Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. - Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.
9. Mwembe: Majani magao mawili, ponda na chemsha ndani ya lita 6 za maji hadi ibaki lita 1. Wape kwa siku moja. Mwembe hutibu: • Homa ya matumbo. • Mafua. • Kinga ya Kideri/Mdondo.
10. Mpera: Chemsha majani au mizizi. Mpera hutibu: • Tumbo • Vidonda na majipu 11. Minyaa (Cactus): Hii ni aina yenye majani manene-hadi kufikia nusu nchi na mapana hadi kufikia upana wa viganja viwili vya mikono.
11.Minyaa hutibu: (Angalia inaunguza au kubabua). • Vidonda. • Ngozi. • Uzazi
12. Pilipili Kichaa:
[a]Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu Mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).
[b] Chukua pilipili 5 za kichaa au ndefu au mbuzi kama ukikosa zote, twanga weka kwenye maji lita 4,wape baada ya kula. Wape kwa siku 5 _Hutibu aina zote za mafua
13.Kitunguu swaumu:
Hutibu Mafua,Typhoid,Kuharisha kinyesi cheupe
Jinsi ya kutumia Unakitwanga kisha uchanganya kwenye maji chuja kwa chujio ili kuondoa nyuzi na uchafu. Kiwango cha kuwapa kitategemeana na idadi ya kuku. Huu ni ushuhuda wa mfugaji alie wahi kutumia kitunguu swaumu kwa kuku wake "["Mimi nilitumia vitunguu vinne nikatwanga kisha nikachanganya na maji glasi moja na nusu zile za plastic kisha nikachuja nikawa nawapa na kijiko Mara mbili kwa Siku nilikuwa namshika mmojammoja nampa ili kuhakikisha wanapata dawa wote nikimaliza nawawekea maji ya vitamin wasipoteze hamu ya kula ukiwapa vizuri Siku mbili tu unaona wanapa nafuu"]
Tumia Dawa Za Asili Kabla Ya Ugonjwa Haujawa Komavu
Kumbuka chanjo kwa kuku ni muhimu sana
#share mara nyingi na Mungu atakubariki na wenzio wapate elimu
#like page
#comment
PATA VITABU VYA MUONGOZO WA UFUGAJI KUKU SOFTCOPY NI 5000 TUNATUMA KWA WHATSAPP AU EMAIL WASILIANASI KWA 0652039671
No comments
Post a Comment